Burudani

Picha, Mshambuliaji wa Man City Sergio Aguero amevunjika mbavu baada ya kupata ajali ya gari

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Mshambuliaji wa Man City Sergio Aguero amevunjika mbavu baada ya kupata ajali ya gari huko Amsterdam,Uholanzi usiku wa kuamkia leo.

Aguero,29, alipanda Taxi akielekea uwanja wa ndege baada ya kuhudhuri a tamasha la msanii wa Colombia,Maluma na ndipo dereva akapoteza mwelekeo na kugonga nguzo pembezoni mwa barabara.
Imeripotiwa kuwa Muargentina huyo alifunga mkanda katika siti aliyokuwa amekaa na ndio uliomsaidia asipate majeraha zaidi.

Mchezaji huyo amepelekwa hospitali kwa ajili ya kupata matibabu na kufanyiwa uchunguzi kama mchezaji wa soka na klabu yake.

Majeraha hayo yanamfanya kukosa mechi ya jumamosi dhidi ya Chelsea na imeripotiwa kuwa anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki 6 mpaka 8.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open