Burudani

Billboard wanasema album ya Eminem imekaa kwenye chati kwa wiki 350 na kuhusu filamu mpya anayotayarisha

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Rekodi imewekwa wiki hii baada ya billboard kutangaza rasmi kuwa album ya Eminem ya mwaka 2005 Curtain Call: The Hits imekuwa album ya hiphop iliyokaa zaidi kwenye chati hizo kuliko album yoyote duniani.

Album ya Curtain Call ilishika namba moja kwenye chati za bilboard 2005 na mpaka sasa imeuza kopi milioni 7, Imekaa kwenye chati za billboard kwa wiki 350.

Album nyingine ya Eminem ya mwaka 2002, The Eminem Show ilikaa kwenye billboard kwa wiki 329 na ya mwaka 2010, Recovery ilikaa kwa wiki 288.

2>>Eminem kwa sasa anatayarisha filamu ya vituko ya mashindano ya rap #Bodied

Eminem anatayarisha filamu ya vichekesho itakayohusu mashindano ya rapa, filamu hii imepewa jina Bodied.

Rapa huyu anahistoria ya filamu hizi baada ya kufanya vizuri kwenye filamu yake ya mwaka 2002 ya 8 Mile,

Filamu hii imeandikwa na mshindi wa mashindano ya Rap Alex “Kid Twist” Larsen, Bodied itaongozwa na director maarufu wa video za muziki Joseph Kahn, ambaye ameshatengeneza video za wasanii kama Eminem, Britney Spears, Taylor Swift, Lady Gaga, U2, filamu hii itatoka kwenye Toronto International Film Festival mwezi wa Tisa.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open