Burudani

Baada ya Rapa Young Dolph kupigwa risasi, Yo Gotti wa lebo ya JAY -Z Ya Roc Nation anatafutwa na polisi

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

 

Rapa Yo Gotti wa lebo ya JAY -Z Ya Roc Nation anatafutwa na polisi baada ya kuhusishwa na tukio la kupigwa risasi kwa rapa mwenzake Young Dolph.

Polisi wa Mjini Los Angeles ‘LAPD’ wamesema Yo Gotti anahitajika kwa mahojiano kuhusu tukio hili sababu wanaushahidi kuwa Young Dolph na Yo Gotti walikuwa pamoja kwenye hoteli ya Loews mjini Hollywood jumanne hii ambapo makundi yao yaligombana mbele za watu.

Polisi wamedhibitisha uwepo wa mashahidi wanaosema Yo Gotti alikuwepo eneo la tukio.

Mwanzoni mwa mwaka huu msanii wa Yo Gotti ‘Blac Youngsta’ alituhumiwa kufyatua zaidi ya risasi 100 katika gari ya Young Dolph mjini Charlotte na baadae Youngsta alijisalimisha polisi.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open