Burudani

Kauli ya Shilole kuhusu mastaa kuwa na mahusiano na ‘ViSerengeti Boys’, Mpenzi wake wa sasa je? kafunguka hapa..

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Akizungumza kwenye kipindi cha #PlanetBongoEARadio Shilole amesema kwa sasa yeye hana mahusiano na wanaume ambao amemzidi umri, kwani mpenzi wake wa sasa ni mwanaume halisi (gentle man) na amemfanya awe na mawazo ya kuwa mke.

Shilole anasema Mwanaume wangu wa sasa sio Serengeti Boy, ni Gentle Man, anajielewa na pia ni mtu mzima, ananifanya mpaka nifikirie kuolewa niwe mke, yani sio Serengeti Boy kabisa, na pia hataki kabisa mambo ya mitandao na ndio maana simuweki wazi.

Shilole amewatetea watu ambao wana mahusiano na wanaume wanaowazidi umri (serengeti boys) na kusemaKwani kitu gani…!! age is just a number, watu wanaangalia mapenzi bwana so its not a big deal kuwa na kiserengeti‘.

Shilole aliwahi kuwa na mahusiano na msanii Nuh Mziwanda na kwa sasa Shilole yupo kwenye ziara ya kutangaza wimbo wake mpya Kigori

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open