Habari

Alichoandika Jaguar baada ya kushinda Ubunge Kenya..

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Staa wa muziki nchini Kenya Charles Njagua Aka Jaguar ameshinda kiti cha ubunge katika jimbo la Starehe nchini Kenya kufuatia uchaguzi mkuu ambao bado unaendelea.

Kwenye IG Yake Jaguar ameandika

“Hakuna linalowezekana bila Mungu, Nawashukuru watu wa Starehe kwa ujasiiri na kuniamini kuwawakilisha bungeni, nawashukuru wote walioniunga mkono , marafiki, familia ambao walikuwa nami wakati wa kampeni. Na Pia nampongeza mpinzani wangu Steve Mbogo, Boniface Mwangi na Mh. Kwenya ambao waliweka kampeni safi. Huu sio ushindi wa Starehe tu bali ni ushindi wa vijana wote nchini Kenya ambao wameona mbele, sasa tuijenge Starehe ile tunayoitaka, Mungu awabariki”

Jaguar ameibuka mshindi wa Jimbo hilo kwa asilimia 53% ya kura zote, huku akifuatiwa na Steve Ndwiga  aliyepata asilimia 31% na Boniface Mwangi akipata aliyepata asilimia 13%.

Ukiachana na Jaguar, wasanii wengine walioko kwenye siasa Afrika mashariki ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Tanzania’ , Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Tanzania’ na Uganda Ni Msanii Robert Kyagulanyi Ssentamu ambaye ni mbunge wa Kyadondo East.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open