Burudani

Picha, Pop staa Justin Bieber akemea UBAGUZI

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Pop staa kutoka Canada Justin Bieber ameunga mkono kampeni na harakati za kupinga Ubaguzi za Black Lives Matter zinazofanywa na watu weusi na weupe nchini Marekani.

Kupitia Instagram yake Justin Bieber ameandika ujumbe kuhusu kupinga na kukata ubaguzi duniani, JB Anasema >>Mimi ni MCanada mwenye ngozi nyeupe, najua sitaweza kujua haswa mtu anajiskiaje kuwa Mwamerika Mweusi ila naweza kusimama na kutumia sauti yangu dhidi ya Ubaguzi, Sababu Ubaguzi Upo kweli na umekuwa mkubwa zaidi wakati kuliko muda wote katika Maisha yangu duniani, Sisi wote ni watoto wa Mungu na tuko SAWA

Justin Bieber ni miongoni mwa wasanii weupe mwenye marafiki weusi wengi zaidi ndani na nje ya Marekani, Kipaji chake kiligunduliwa na kutambulishwa duniani na mtu mweusi ‘Usher Raymond’.


#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open