Burudani

Kauli ya Msaga Sumu kuhusu kuweka Meno Bandia ili kufunika Mapengo…

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Msanii maarufu wa muziki wa Singeli Msaga Sumu amesema hana mpango wa kwenda kuweka meno ya bandia ili kuziba mapengo akidai hicho ndiyo kitambulisho chake cha kumtofautisha na wengine.

Msaga Sumu anasema ‘Walishatokea wadau wakataka kunipeleka nchini Ureno kwa ajili ya kuwekewa meno yale yenyewe kabisa kama haya ambayo ninayo lakini mimi mwenyewe nikasema hamna isitoshe watu wengi walishanipiga hela kwa kunitumia mimi, lakini sasa hivi nikishuka tu sehemu watu wanajua ndiyo mwenyewe kwa sababu ya mapengo yangu‘.

Staa huyu wa Singeli amesema hakumbuki mpaka sasa ni meno mangapi yametoka katika kinywa chake kwa kuwa watu wanaotoka pande za Kusini huwa na meno yanayotoka yenyewe.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open