Burudani

Peter Okoye ajitoa tena kwenye kundi la P Square,sababu ziko hapa

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Habari mbaya kwa kundi la P Sqaure baada ya Peter Okoye kujitoa rasmi kwenye kundi hilo,

Mtandao wa Linda Ikeji umeripoti kwa asilimia 100 kuwa Peter Okoye ametuma barua ya kujitoa kwa wakili wao Festus Keyamo, akihitaji kuvunjwa kwa makubaliano baina yake na P-Square.

Ndani ya barua hiyo, Peter ambaye kwa sasa anajiita Mr. P, ametoa sababu za kujitenga na P Square (Paul Okoye) pamoja na Meneja wao (Jude Okoye) akidai Paul hakuwa tayari tena kuendelea kushirikiana naye kikazi, kiasi cha kufuta mpango wa ziara yao nchini Marekani bila kumjulisha.

Sababu nyingine iliyosababisha P Square kusambaratika ni mgogoro wa kifamilia uliofikia pabaya kiasi cha kaka yake, Jude kutishia kumuaa Peter pamoja na mkewe Lola.

Peter alisema “Jude threatened me to come with my coffin Whenever he sees me around his house.” 

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open