Burudani

PitBull atuma ndege yake binafsi kuokoa wagonjwa wa Saratani katika visiwa vya Puerto Rico

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

 

Baada ya visiwa vya Puerto Rico kuathirika vibaya na kimbunga ‘Maria’ , rapa Pitbull ametuma ndege yake binafsi kubeba wagonjwa wa Saratani ili waletwe kwenye hospitali zingine kwaajili ya Matibabu ya Chemotherapy.

Kimbunga hichi kimeharibu huduma za maji, umeme na mpaka sasa hospitali 11 tu kati ya 69 za kisiwa hicho ndio kuna umeme kitu ambacho kinahatarisha maisha ya wagonjwa.

Kwenye hospitali ya San Juan, watu wawili wamefariki baada ya mashine zinazowasaidia kupumua kuzimika baada ya jenereta kuisha mafuta ya Diesel,
Meya wa San Juan Carmen Yulín Cruz watoto 12 bado wanategemea umeme na bettrey ili kupumua katika hospitali ya watoto ya San Jorge Children’s Hospital.
Msemaji wa PitBull kaongea na CNN nakusema “Thank God we’re blessed to help. Just doing my part.”
#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open