Burudani

Hii ndio simu itakayovunja rekodi ya kuchaji betri kwa haraka zaidi…

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Kama umekuwa ukitafuta simu kali ambayo itakuwezesha kufanya mambo mengi bila kuhitaji kuichaji mara kwa mara basi “Tecno Mobile” wanakusogezea hii inaitwa Tecno L9 Plus, simu hii itakuwa na uwezo wa kuchaji fasta kupita kiasi. Unaambiwa kuchaji asilimia 5 tu kutakuwezesha kupiga picha takribani 1,000. Tazama video hapa chini ikifunguliwa kutoka kwenye boksi na kucheki sifa ilizonazo.

Tecno L9 Plus inatarajiwa kuingia sokoni hapa nchini katikati ya mwezi huu wa Machi na habari njema kutoka Tecno ni kwamba sasa unaweza kuweka oda yako mapema ambapo mteja ataweza kujipatia kifurushi cha zawadi. Baadhi ya zawadi zitakazogawiwa ni Boom Headphones, mabegi ya mgongoni na nyingine nyingi.

Unachotakiwa kufanya ni kufika katika maduka yafuatayo na kulipa kiasi cha shilingi 30,000 (Elfu thelathini) kama malipo ya awali na moja kwa moja utajipatia kifurushi cha zawadi. Muda wa kushiriki ni kuanzia 10.03.2017 hadi 20.03.2017.

Kwa taarifa zaidi nakusihi kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno kujua zaidi.

Facebook: https://www.facebook.com/TECNOMobileTanzania/

Instagram: https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/

Twitter: https://twitter.com/TECNOMobileTZ

Weka Comments Hapa

Open