Burudani

2 Chainz mahakamani baada ya kushindwa kumalizia malipo ya gari lake la kifahari

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Rapa 2 Chainz anaelekea kupoteza gari lake la kifahari aina ya Rolls-Royce baada ya kushindwa kutuma malipo ya kila mwezi ya gari hilo.

Kampuni ya Highline Holdings Group wanasema 2 Chainz aliuziwa gari aina ya Rolls-Royce Phantom Drophead ila mpaka sasa rapa huyu hajamalizia pesa hizo kitu ambacho ni tofauti na makubaliano yao.

Highline iliongea na kampuni inayomiliki gari hii waliuze kwa dola $262,212 bei ambayo 2 Chainz alikubali kulipa ila mpaka sasa hajamalizia dola $18,317,

Highline wanasema 2 Chainz anagoma kumalizia pesa hizo na wameenda mahakamani kudai haki yao, Inasemekana 2 Chainz hajapata hata nafasi ya kuendesha gari hilo baada ya kuwa na ziara ndefu ya muziki huku akiwa na mguu mbovu.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open