Burudani

Priyanka Chopra aitamani nafasi ya kuigiza kama Super Hero….

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Mwigizaji Priyanka Chopra anaiteka Hollywood kwa kasi baada ya kutoka kwa filamu ya BAYWATCH aliyofanya na Dwayne The Rock Johnson sasa staa huyu kutoka Bollywood ametaja nafasi ya Super Hero anayotaka kucheza Hollywood.

Priyanka ameongea na Jarida la OK nakusema angependa acheze filamu za Batman ila aigize kama BATGIRL.

Priyanka amekuwa akisaka nafasi ya kung’ara Hollywood na sasa labda anaitamani nafasi ya kuigiza kwenye filamu ya Joss Whedon Batgirl, iliyotangazwa kutoka mwaka 2018.

Priyanka Chopra anategemea kuanza kuigiza msimu wa tatu Quantico, kwenye husika yake kama Alex Parrish.
#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open