Burudani

4.44 Sio album ya Jay Z, ni filamu mpya, staa huyu kutoka Afrika Mashariki yupo….

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Mashabiki wa Hip Hop walipata shauku kubwa baada ya tetesi kusamba kuwa “4:44” ni album mpya ya Jay Z, imethibitishwa kuwa 4.44 ni filamu mpya.

Matangazo ya 4.44 kwenye tovuti ya Tidal yanahusu filamu mpya iliyofanywa na mastaa Mahershala Ali uliyemuona kwenye (Moonlight), Lupita Nyong’o uliyemuona kwenye (12 Years A Slave), na Danny Glover (The Color Purple).

Promo ya filamu hii yenye dakika moja ilionekana kwenye tovuti ya Tidal na kurushwa tena kwenye mchezo wa tatu wa fainali za NBA 2017.

CEO Wa kampuni ya Sprint Marcelo Claure alitoa taarifa ya filamu hii 4:44  kwenye Twitter yake…

“Excited to bring [Sprint] customers exclusive content through our partnership with [Tidal] – more news coming tomorrow!!”

Kampuni ya Sprint inamiliki asilimia 33% ya hisa za Tidal ya Jay Z.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open