Burudani

50 Cent kwenye matatizo baada ya kutumia picha zake zilizopigwa na mtu mwingine bila kibali

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Mpiga picha Christopher Pasatieri amefungua kesi ya madai dhidi ya 50 Cent baada ya rapa huyu kutumia picha alizopigwa na Christopher kutangaza bidha zake kwenye kurasa yake ya instagram.

50 Cent alitumia picha alizopigwa na Christopher kutoka kwenye show ya June 2014 na kuziweka Instagram huku akitaja bidha zake kama SMS Audio headphones na show yake ya Tv ya “Power.”

Mpiga picha Christopher anataka fidia ya pesa sababu picha hizi zimejizolea zaidi ya LIKES 42,000 kwenye kurasa ya 50 Cent.

Christopher amefungua mashtaka dhidi ya club ya Citi Field iliyotoa picha hizo kwa 50 Cent bila ruhusa na kibali baada ya kufanya show na kundi lake la G-Unit

#SammisagoNEWS

 

 

 

 

Weka Comments Hapa

Open