Burudani

Alichoandika Mh Joshua Nassari kuhusu Unafiki wa wasanii wa Bongo Fleva, Majibu ya Nikki Wa Pili yako hapa

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia chama cha  CHADEMA  ,Mh Joshua Nassari  amekosoa mtindo wa baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva kuwa wanaharakati zaidi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kwenye nyimbo zao

Kupitia kurasa yake ya Twitter,Mh Joshua Nassari  aliandika> Ni dhahiri Tz tuna wasanii wanafiki sana ambao ni mizigo kwa jamii. Msanii anaimba mapenzi 24/7 halafu huku kwenye mitandao ya kijamii anajifanya activist, kutwa amegeuka mwanafalsafa. Sasa kule ambapo una audience kubwa si ndipo pa kuyasemea haya unayoyahubiri huku TL???!

Baada ya post hii msanii wa HipHop Nikki wa Pili alimjibu kwa kuandika

Nikki Wa Pili>Usikae kiharasa tumia akili yako, alafu wasanii wanatafuta hella waende maisha yao

Ata baada ya Mh Nasari kuandika >Nimemtaja mtu kwenye tweet yangu chief??! Mbona wapo wengi….

Bado majibu ya Nikki wa Pili yalizidi kumiminika, Nikki aliandika

Nikki Wa Pili>Wimbo wangu wa mwisho unaitwa kihasara, wakati wa kampeni wanasiasa pande zote walilipa wasanii kuimba nyimbo za matusi na kashfa eti leo wanashauri wasanii waelimishe, na vijana wasiopenda kuchambua mambo hujitokeza kushangilia, fikiri kwa akili yako bro

Nikki Wa Pili>Wanasahau good boy,kiujamaa,niaje ni vipi, kihasara, madaraka, kaributena,stimuzimelipiwa, luck me….tatizo vijana hawapendi kufikiri kwa akili zao wanapenda mawazo ya kuokota

Je unadhani Mh Joshua Nassari  alikuwa akiongelea msanii au wasanii gani ?

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open