Mchezaji mkongwe Andrea Pirlo,38, amesema atastaafu Soka baada ya mkataba wake kumalizika katika Klabu ya New York City mwezi December 2017.

Andrea Pirlo amekuwa akipitia wakati mgumu uwanjani toka kuumia goti na mpaka sasa ameweza kucheza game 15 tu katika game 32 za timu ya New York City

Akiongea na gazeti la Italia la La Gazzetta dello Pirlo anasema >Muda umefika, kila siku una matatizo ya mwili na huwezi kufanya mazoezi, kwa umri wangu sasa ni sawa kusema imetosha sasa, sio lazima nicheze mpaka nikiwa na miaka 50,nitafanya kitu kingine”.

Pirlo pia amesema bado hajafanya maamuzi kamili kuhusu tetesi za yeye kuwa kocha na kwenda kuwa msaidizi wa kocha wa Chelsea Antonio Conte

Baada ya miaka 25 uwanjani sasa naweza kukaa nyumbani na familia yangu.