Burudani

Rapa Birdman awatolea POVU wanaozidi kuongelea beef lake na Lil Wayne

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Rapa na mdau mkubwa wa muziki USA ambaye pia ni miongoni mwa wamiliki wa lebo ya Cash Money Birdman amewatolea POVU wanaozidi kuongelea beef lake na mtoto wake wa kambo Lil Wayne.

Kupitia Instagram live Video Birdman anasema “Wale mnaosema mara Lil Wayne hichi, mara Lil Wayne kile, Lil Wayne ni mtoto wangu, nime mlea, alikuwa hana kitu, nimefanya awe na vitu na kuwa mtu, unadhani sitaweza kuweka mambo yake sawa, endeleeni kunitazama Mimi ni Master Mind mkali sana”.

Birdman hapa anaongelea kusukumwa na wasanii wakubwa kama Rick Ross ili alipe dola milioni 51 anazodaiwa na rapa Lil Wayne.

Kama hufahamu Beef la Lil Wayne na Birdman lilianza December 2014, Wayne alipoomba kutolewa kwenye lebo ya Cash Money na baadae kusema anadai lebo hio pesa zaidi ya dola milioni 51 na kwamba Birdman anazuia album ya Carter 5 kutoka.

Beef Lina Endelea

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open