Habari

Breaking;Mbunge wa Singida Mashariki, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amepigwa risasi Dodoma

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Mbunge wa Singida Mashariki, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amepigwa risasi akiwa Dodoma.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchana akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa ametoka bungeni na kwenda nyumbani kwake kwa ajili ya kupata chakula cha mchana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba Mh. Lissu kwa sasa amekimbizwa hospitali kwa ajili ya kupata huduma na sasa yupo chumba cha upasuaji.

Mwenyekiti wa CHADEMA,  Taifa naye amesema Lissu yupo hospitali ya General.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open