Burudani

Video mpya ya Busta Rhymes,walibidi warekodi vipande vya Vybz Kartel akiwa jela, Itazame video ya ‘Girlfriend’ hapa

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Hii video mpya ya rapa mkongwe Busta Rhymes Ft Vybz Kartel na Tory Lanez ‘Girlfriend’ Itazame hapa

Rapa mkongwe mwenye album Tisa kwenye mkanda wake ameanza kurekodi album yake ya 10 na tayari ametoa video aliyofanya Jamaica ya wimbo wake wa ‘Girlfriend’ akiwa na Vybz Kartel na Tory Lanez

Kwenye Video hii iliyoongozwa na Bussa Bus na Benny Boom anaonekana staa mwingine wa Dance Hall

Kabla ya kwenda kumalizia video hii, Busta Rhymes alibidi azame jela aliyofungwa msanii Vybz Kartel na kurekodi vipande vyake akiwa kwenye chumba kidogo kwenye jela hio.

Wasanii wengine kwenye video hii ni pamoja na Ninja Man, Junior Reid, Foota Hype, Spice, na Bounty Killer.

Hii inatajwa kuwa album ya mwisho ya Busta Rhymes na mpya toka mwaka 2012 alipotoa Year of the Dragon.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open