Burudani

Cardi B awachana wanaosema anakopi mitindo ya wasanii ya kuRAP

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Rapa Cardi B ambaye kwa sasa wimbo wake wa Bodak Yellow unashikilia nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100 amefunguka kuhusu wanaosema ameiba mtindo wa kurap wa msanii Kodak Black na kuutumia kwenye wimbo wake wa Bodak Yellow

Akiwa kwenye jukwaa kwaajili ya show Cardi alisema >Kwa yoyote anayesema ooh Cardi umeiba mtindo wa Kodak, mara nimekopi huyu, mara nimemkopi yule, sasa nini, naweza kuchukua mitindo yote ya wasanii unaowapenda, ipo siku nitaimba kama Kodak,siku nyingine kama Meek Mill , siku nyingine kama Migos, sijali, sababu mwisho wa siku natengeneza pesa”.

Cardi B amekuwa na mafanikio makubwa baada ya ya kutajwa kuwania tuzo tisa katika tuzo za HipHop za BET 2017 na kuweka record ya kuwa msanii wa pili wa kike wa hiphop mwenye wimbo ulioshika namba moja kwenye billboard bila colao, awali rekodi hii alikuwa nayo Lauryn Hill pekee toka November,14,1998 na wimbo wa“Doo Wop (That Thing),”.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open