Burudani

Mambo 12 yakufahamu kuhusu MC mkali wa Kike kwa sasa Cardi B

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Baada ya Rapa Cardi B kuweka rekodi ya kuwa msanii wa rap wa Kike wa pili kushika namba 1 kwenye chati za Billboard Hot 100 Bila Colabo kupitia wimbo wake wa #BodakYellow wengi wametamani kujua machache kuhusu MC huyu. 

-Fahamu kuwa rekodi hii ilikuwa ikishikiliwa na rapa Lauryn Hill toka November,14,1998 na wimbo wa“Doo Wop (That Thing),”.

-Jina halisi la Cardi ni Belcalis Almanzar, anatokea mitaa ya Bronx, wazazi wake wanaishi Trinidadian/Dominican

-Wimbo wake wa “Bodak Yellow” umetokana na flow kali ya Msanii  Kodak Black aliyoitumia kwenye wimbo wake wa “No Flockin,”

-Baada ya umaarufu kwenye muziki Cardi alijaribu tena karata yake kwenye kipindi cha Tv cha  Love & Hip-Hop, na kutokana na utundu wake aliweza kuvutia sana watazamaji mpaka  December 2016 alipotangaza kujitoa.

-Cardi B alifanya kazi kama STRIPPER Kwenye migahawa ya watu wazima mjini New York toka akiwa na miaka 18 mpaka mwaka 2015 alipoacha na kuwa mshehereshaji wa club za usiku tu.

-BET walimpa mchongo mkubwa wa Tv show ya Being Mary Jane, nakuigiza kama Mercedes akiwa na staa mkubwa Gabrielle Union.

-Kabla ya kupenya vizuri kwenye muziki Cardi B alifanya Mixtape Mbili, Gangsta B—h Music Vol.1 na Gangsta B—h Music Vol. 2 

-Thamani ya Cardi B  ilikuwa dola $600,000 mpaka September 2017 ila baada ya mafanikio ya ‘Bodak Yellow’ imepanda mpaka kuwa dola milioni $4m.

-Mafanikio ya wimbo wake wa ‘Bodak Yellow’ yalimpa nafasi ya kufanya show ya Made in America August 2017na ndipo alipokutana na JAY-Z Na Beyonce.

-Cardi B na Nicki Minaj hawana BEEF

-Mpenzi wake Cardi B ni msanii wa kundi la Migos #Offset

-Wimbo wake wa Bodak Yellow ulishika namba moja kwenye Billboard 100 September 2017

#SammisagoNEWS

 

 

Weka Comments Hapa

Open