Burudani

Mambo nane aliyosema Cardi B katika interview ya jarida la Rolling Stone

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Cardi B amesema hajaamini mpaka sasa toka amepokea simu kuwa atafanyiwa interview na jarida la Rolling Stone na kutokea kwenye kurasa ya mbele ya jarida hilo katika toleo lao la November 2017 ‘The Hot Issue’.

Haya ni mambo nane makubwa aliyofunguka

Cardi B kuhusu Album> Nimekamilisha nyimbo 7 ambazo nazipenda, sijui kitakacho badilika ndani ya mwezi mmoja kutoka sasa, sio furaha sana kwangu kufanya muziki sababu akili yangu ina mambo mengi”.

Cardi B kuhusu Umaarufu>Siwezi tena kurudisha maisha yangu nyuma, tayari nimeshakuwa nyota, mtu maarufu, ni bora niendele tu kuwa hivi, nitengeneze pesa, watu wataongea ujinga kila siku ila siwezi kujivua umaarufu.

Cardi B kuhusu Beef za Rap: Sio wasanii  a kike ndio wanazitaka, ni Mashabiki ndio wanataka BEEF Tu  

Cardi B kuhusu Mwelekeo wa Muziki wa RAP: Ni huzuni sana kusema hichi na sitaki kuwa mtu wa kukisema ila kizazi chetu kinapenda kufata TREND, wanapenda kulewa na kuwa na mizuka, wanapenda dawa za kulevya, ndio wnachotaka , hawataki kufikiria sana unachosema

Cardi B kuhusu Mchumba wake OFFSET:Tuna saidia sana, naweza muuliza chochote kama ‘Je nachofanya hapa ni sawa, je unadhani hapa nachezewa mchezo flani ?’ 

Cardi B kuhusu Maisha yake ya mbele: Natakikwa kutengeneza pesa kwaajili ya familia yangu na familia yangu ya mbele, nafikiria miaka 25 kutoka sasa, nafikiria watoto wangu , mume wangu na nyumba yangu

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open