Burudani

Cardi B kafunguka kuhusu Ujio wa Album mpya, kukutana ba Beyonce

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Rapa ambaye kwa sasa rekodi yake ya  “Bodak Yellow (Money Moves),”  inafanya vizuri kwenye chati za Billboard, Cardi B amefunguka kuhusu ujio wa album yake ya kwanza.

Cardi B anasema “Nina album inakuja, nina wasi wasi kidogo na kutoa album hii, nidhani ni album kali,  kila mtu anasubiri kuona nitakachofanya, najiamini na najua nitafanya mambo makubwa”.

Kuhusu heshima kutoka kwa wasanii wengine, anasema “Nimepitia mambo mengi sana na sasa napata heshima kutoka kwa wasanii wengine na kupata kila nilichowahi kutaka”.

Beyoncé amenionyesha mapenzi, nilishanga alionyesha kunipenda,  “Ah! I met Beyoncé!”, Cardi alikutana na Bey kwenye show ya Made in America.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open