Burudani

Shabiki aliyepigwa ngumi ya jicho na Chris Brown kalipwa

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Chris Brown anaendelea kumaliza vimeo vyake mahakamani, wiki hii staa huyu wa Rnb amemlipa dola 70000 mwana dada Liziane Gutierrez aliyelalamika kupigwa ngumi ya jicho na Chris Brown mjini Las Vegas

Liziane Gutierrez anasema alikuwa akijaribu kumpiga picha Chris kwenye party moja Las Vegas katika hotel ya Palms na ndipo Chris Brown alipompiga ngumi ya jicho.

Polisi hawakumkamata Chris au kufungua mashtaka yoyote ila baadae dada huyu alifungua kesi ya madai kuwa alipata madhara jichoni kutokana na kitendo cha Chris na kutaka kulipwa fidia.

 

Chris Brown alijitetea kwa kusema mwanamke huyo ni MBAYA sana hawezi kuwa kwenye party yake at kuthubutu kuingia kwenye chumba cha hoteli yake.

 

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open