Burudani

Kauli ya Chris Brown kuhusu kusifia matumizi ya dawa za kulevya na Kusema vibaya mitandaoni

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Week hii staa wa rnb Chris Brown amefunguka mambo mawili makubwa kwenye maisha yake kwa sasa ambayo ni tuhuma za kusiia matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kusemwa vibaya mitandaoni.

Chris Brown akihojiwa aliulizwa kuhusu promo ya dawa za kulevya kwenye wimbo wake wa “Pills & Automobiles’, Chris anasema ‘Ni wimbo mrahisi wa kula bata na kuburudika, maneno niliyotumia ni maneno yetu ya mtaani, sikumaanisha watu watumie vidonge kulewa, ni vitu tunafanya wakati wa kula starehe ndio vimeimbwa humo” 

Chris pia amefunguka juu ya kukaambali na Blogs zinazomchafua na kusema “Nimejifunza kukaa mbali na hayo mambo, Blogs na watu wataongea tu ila nikijibu mimi ujue kimenidhuru mimi , ila kama sihusiki na kilichosemwa basi sitasema lolote, mambo mengine yoyote ni Ujinga tu”

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open