Burudani

Chris Brown athibitisha kumtamani Jennifer Lopez, yuko tayari kwa lolote

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Chris Brown amethibitisha kuwa huwa anamtamani sana Jennifer Lopez na hana aibu kusema hilo.

Chris Brown akihojiwa na Angie Martinez alisema “J Lo ni Nomaa sana, nampenda na nina mtaka” alipoulizwa kuhusu utofauti wake na J Lo kwa Umri ambao ni miaka 20, Chris alisema “Sijali ata akiwa ni miaka 70 anaweza kuwa na mimi muda wowote”

Chris Brown ambaye amewahi kuwa na mahusiano na Rihanna na Karruche Tran,amesifia mahusiano ya kikazi kati yake na J LO.

Chris anasema “Nimeandika mashairi zaidi ya mara moja kwenye album zake, niliwahi kwenda kwake kuandika muziki, nilikuwa kibiashara zaidi, ila ukimtazama na macho ya moyo wako lazima utasema You look good”

Chris amesema hajawahi kumwambia J Lo uso kwa Uso kuwa anamtaka, kwa sasa J Lo yupo na mpenzi wake Alex Rodriguez.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open