Michezo

Updates, Conor McGregor vs Floyd Mayweather Jr….

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Mpiganaji wa mchezo wa MMA ‘Mixed Martial Artist’ Conor McGregor amemtusi bondia maarufu Floyd Mayweather Jr baada ya staa huyu kushindwa kuonana naye mjini Las Vegas kuongelea pambano lao.

Wiki iliyopita Floyd alimwambia Conor kuwa kama anataka pambano kweli basi awasiliane na watu wake sio yeye binafsi.

Conor McGregor ambaye amekuwa akitaka pambano la ngumi na Floyd Mayweather Jr amesema walipanga kukutana mjini Las Vegas kuzungumza ila Floyd hakuonekana.

Conor McGregor ametumia maneno haya kumuelezea mpinzani wake Floyd’s a b***h and he’s petrified

Pambano hili limekuwa likishabikiwa na wapenzi wa ngumi za kulipwa na MMA ila mpaka sasa hakuna aliyeweka pesa za kutosha kumshawishi Floyd Mayweather Jr kuingia uwanjani na Conor McGregor.

Tazama na Sikiliza Interview Za Kuburudisha Kwenye Channel Yetu,Bonyeza HAPA

Weka Comments Hapa

Open