Burudani

Huyu ndiye aliyependekeza Diamond Platnumz kutayarisha wimbo wa kombe la dunia

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Msanii wa kimataifa kutoka Tanzania anayefanya muziki wa Bongo Fleva na Pop Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii wa kimataifa watakao tayarisha nyimbo za kombe la dunia 2018.

Diamond atatayarisha wimbo wa Afrika Mashariki kwaajili ya 2018 soccer World Cup nchini Urusi.

Jina la Diamond lilipendekezwa na aliyekuwa Director wa Ubunifu wa MTV Base Tim Horwood ambaye alipewa mchongo huu na Coca-Cola kutafuta wasanii kwaajili ya kazi hii.

Diamond atakuwa na Cassper Nyovest wa S.A, Ethiopia inawakilishwa na Sami Dan, Mozambique ni Lizha James na Uganda ni Ykee Benda, wimbo utahusisha rangi za nchi zote hizi.

Nyimbo hizi zitatengenezwa kubadilisha mtazamo mbaya wa nchi za Afrika uliojengeka sehemu tofauti duniani.

Wimbo huu utakuwa ukichezwa pamoja na wimbo wa FIFA World Cup wa Official Coca-Cola World Cup Anthem Colours uliofanywa na Jason Derulo.

FIFA World Cup inaanza June 14th mpaka July 15th 2018 nchini Urusi, zinacheza nchi 32, Africa inawakilishwa na Tunisia, Nigeria, Morocco, Egypt na Senegal.
Christian Bella Afunguka kuhusu Collabo na Mafanikio ya Diamond Platnumz

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open