Burudani

Diamond alivyodili na jamaa flani aliyemtongoza Zari instagram….

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Kupitia kipindi cha #LeoTenaClouds FM Diamond na Zari walikuwa wakiongelea 40 ya mtoto wao wa pili Prince Nillan na Diamond aliweka wazi kuwa bado kuna wanaume wanamyemelea Zari.

Diamond kwenye radio alisema “Kulikuwa na nyendo za mtu mmoja nilishasikia nikasema sasa mambo ya kusumbuana kupiga simu Kigoma tena ya nini,Zari akamblokia zake mbali, mwanzo kulikuwa na watu wanaojifanya wao wako karibu sana, kujifanya wao ndio wanamwelekeza ‘Diamond anafanya hivi na hivi, yaani unajua kuna watu wengine wana mambo ya ushamba wanahisi wakikumaliza wanatengeneza nafasi zao wenyewe, lakini nikakaa nikasema, kwa suala hili dogo tena mtu mmoja tuanze kupiga simu Kigoma haitakuwa vizuri,”

Diamond na Zari  walisema wanamakubaliano ya kutoshika simu zao kwakuwa husababisha ugomvi sababu wao ni watu maarufu na hupokea mambo mengi kutoka kwa watu.

Tazama na Sikiliza Interview Za Kuburudisha Kwenye Channel Yetu,Bonyeza HAPA

Weka Comments Hapa

Open