Burudani

Disney imethibitisha kubadilisha rangi ya ngozi za waigizaji, Wahindi walalamika kutengwa

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Kampuni ya burudani ya Disney imethibitisha kubadilisha rangi ya ngozi za waigizaji weupe ili kuigiza kwenye filamu ya Aladdin kama watu wenye asili ya Ki-Asia.

Disney imesema ilishindwa kupata waigizaji wengi zaidi wenye Asili ya Asia kuigiza sehemu zote za filamu hii mpya ya Aladin na kupelekea kuwapaka MAKEUP waigizaji wa kizungu ili wawe na rangi za watu wa Asili ya Ki-Asia ili waigize kwenye filamu hii iliyotayarishwa Guy Ritchie.

Disney imesema filamu hii mpya inawatu wa asili tofauti sana kutoka maeneo tofauti duniani, walitumia njia nyingi kuhakikisha kila jamii inawakilishwa sawa na hakuna ubaguzi uliotokea.

 

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open