Habari

Dkt Kigwangala; Serikali ina mkakati wa kuongeza mashine tatu za vipimo vya vinasaba (DNA)

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Serikali imedhamiria kununua mashine tatu za vipimo vya vinasaba (DNA) ili zitumike katika maabara za Kanda na hivyo kusogeza huduma karibu na wananchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala wakati akijibu swali la Mbunge wa Chumbuni Mhe. Ussy Pondeza kuhusu ucheleweshwaji wa matokeo ya uchunguzi wa sampuli ikiwemo sampuli za makosa ya jinai.

Dkt Kigwangala amesema kuwa Serikali ina mkakati wa kuongeza mashine hizo ili kuwezesha uchunguzi kufanyika kwa wakati kwa vielelezo vya makosa ya jinai ikiwa ni pamoja na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

Aidha, Dkt. Kigwangala amesema kuwa sampuli za uchunguzi wa makosa ya jinai zinachukuliwa toka maeneo ya matukio hivyo uchunguzi wake unaweza kuchukua muda zaidi kutegemeana na aina ya sampuli na eneo zilipotoka.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open