Burudani

Album mpya ya Eminem imepata tarehe rasmi ya kutoka.

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Taarifa nzuri kwa wampenzi wa muziki wa HipHop ni kuwa Album mpya ya Eminem imepata tarehe rasmi ya kutoka.

Kwa Mujibu wa Hits Daily Double, Album mpya ya Eminem itatoka rasmi November 17, 2017.

Hivi karibuni pamekuwa na stori nyingi kuhusu ujio wa album hii, baada ya producer Denaun Porter kuthibitisha imekamilika na baadae kusema alikuwa akitania tu na kwamba taarifa ile sio yake kutoa.

Denaun Porter ni producer aliyesajiliwa na lebo ya Shady Records ya Eminem.

Eminem anatimiza miaka 45 October 17 2017 na hii itakuwa album yake ya Tisa toka ‘The Marshall Mathers’ LP 2 ya mwaka 2013.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open