Michezo

Idadi kamili ya waliohudhuria,waliolipia na Mauzo ya Ticket ya pambano la Floyd Mayweather Vs Conor McGregor

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Namba kamili za pambano la Floyd Mayweather na Conor McGregor zimetolewa rasmi na imetajwa kuwa mauzo ya Ticket  yameingiza dola za Kimarekani Milioni 55.4 na kuwa pambano la pili la ngumi kuwa na mauzo makubwa zaidi.

Rais wa UFC Dana White alitabiri mauzo ya Ticket yatakuwa dola milioni 70.

Mpaka sasa pambano linaloshikilia nafasi ya kwanza kwa mauzo makubwa ni la Mayweather Vs Manny Pacquiao la mwaka 2015 lililoingiza dola milioni 72.2.

Waliohudhuria pambano la Conor McGregor Vs Floyd Mayweather ni watu 13,231 na waliolipia na kutazama kwenye Tv kupitia PayPerView ni watu milioni 6.5 ikiwa ni watu milioni 2.2 zaidi waliotazama katika tukio lolote duniani.

Nchi 200 waliweza kulipia na kutazama, Uingereza walilipia dola 19.95 [TZ Sh 42000], na Marekani kila nyumba ililipia dola 100 [Tz Sh 224200] kutazama pambano.

Watu milioni 2.93 walitazama pambano hili bila kulipia, kwa kuibia kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Youtube, Periscope na Twitch

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open