Michezo

Floyd Mayweather amekubali kupigana Conor McGregor, hizi ndio pesa atakazo lipwa….

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Bondia Floyd Mayweather amekubali kupigana na UFC Champion Conor McGregor kwenye pambano la ngumi la light-middleweight mjini Las Vegas mnamo 26 August, 2017.

Mayweather, 40, amethibitisha pambano hili kufanyika mwaka huu kupitia video fupi aliyoweka twitter nakusema “It’s official.” na McGregor, 28, amesema “The fight is on.

Floyd Mayweather anategemea kutengeneza kati ya dola za kimarekani milioni $200 mpaka $300 million na McGregor atalipwa dola za Kimarekani milioni $100m (£78.4m), hili limetajwa kuwa pambano lililolipa zaidi wapiganaji kwenye historia ya ngumi duniani.

Mayweather alistaafu ngumi kwa mara ya kwanza mwaka 2008 baada ya mapambano 39 ila baadae alirudi tena kucheza ngumi na kustaafu kwa mara ya pili mwaka 2015 baada ya mapambano 49 bila kupigwa hata moja.

Exclusive, Stereo Afunguka kuhusu kujiunga WCB WASAFI, Aliyesababisha Colabo na Rich Mavoko,Nani mkali kati ya Godzila Na Wakazi ?

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open