Burudani

Future sasa anatukana familia nzima ya Ciara

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Baada ya kuona mtoto wake wa kiume ‘Baby Future’ analelewa vizuri na mume wake wa Ciara ‘Russel Wilson’ Ex wa Ciara ‘Future’ amezidi kutoa maneno ya kejeli na matusi kwa familia hio.

Katika mixtape ya Future na Young Thug “Super Slimey” kwenye wimbo wa “REAL LOVE” rapa Future ana Diss familia hio kwa kusema “Timu ya Russell ya The Seattle Seahawks imefilisika na yuko tayari kuinunua, yeye ndio alimuhonga zaidi Ciara, sasa Ciara kachoka na hana cha kufanya, pia anaweza kumshtaki tena akitaka ila ndio hivyo kasha toa povu lake”.

Inasemekana Future hajapenda Ciara kuwa na masiha ya familia aliyonayo wakati yeye kukicha yupo na mwanamke mwingine.

Video,Mwili wa Justin Bieber umejaa tattoo

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open