Burudani

Gucci Mane atolewa kwenye orodha ya watu hatari wa kuangaliwa na kuchunguzwa zaidi.

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Miaka miwili kabla ya adhabu yake ya kuwa chini ya uangalizi mkali wa polisi na mahakama kuisha, rapa Gucci Mane atafutiwa rasmi adhabu hio mnamo September 19.

August 23 Jaji Steve C. Jones alitia saini ombi la wakili wa Gucci la kumtoa kwenye orodha ya watu wanaoangalia na kuchunguzwa muda wote na polisi baada ya kutoka jela.

Gucci alitakiwa kuwa chini ya uangalizi mkali wa polisi kutokana na kosa lake la kumiliki silaha bila kibali akiwa tayari ni mtu aliyehukumiwa kwa kosa na kutumikia kifungo mwaka 2014.

Polisi na Mahakama waligundua kuwa baada ya rapa huyu kutoka jela alibadilisha sana maisha yake, alihusika sana kwenye maswala ya muziki na kujipanga kufunga ndoa huku akitayarisha kitabu chake cha The Autobiography of Gucci Mane kinachotoka Sept. 19.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open