Burudani

Kanye West na JAY-Z kukaa kwenye mezi moja ili kumaliza beef lao

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Mtandao wa TMZ Umesema rapa na mfanya biashara mkubwa Marekani Kanye West ameomba mkutano wa Uso kwa Uso na mshkaji wake JAY-Z Ili kumaliza Beef lao.

Beef hili lilikolea baada ya Kanye West kulalamikia familia ya JAY-Z Na Beyonce kuwa wanatenga familia yake na kwamba watoto wao wawili hawajawahi kucheza pamoja.

Jigga alijibu mashambulizi kupitia wimbo wake wa “Kill Jay Z” katika album ya 4:44, na baadae kwenye mahojiano na RapUp JAY-Z Alisema “Tatizo langu na Kanye sio yeye kutoka TIDAL, Tatizo ni pale alipoanza kuhusisha familia yangu kwenye majukwa ya muziki, hapo ata yeye anajua alikosea”.

JAY-Z pia alimalizia kwa kusema kwenye maisha yake hajawahi kuzuia HUSTLE za mtu, ni uamuzi wa Kanye Kutoka au kubaki TIDAL.

Mkutano huu utafanyika kwa siri na inasemekana patakuwa na magwiji wa HipHop kuwapatanisha mastaa hawa.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open