Burudani

Jay Z amekuwa rapa wa kwanza kuwekwa kwenye Songwriters Hall Of Fame….

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Mmiliki wa lebo ya Roc Nation hiphop staa Jay Z amekuwa rapa wa kwanza kuwekwa kwenye Songwriters Hall Of Fame.

Jay Z yupo kwenye orodha ya watu watakao pewa heshima hio mwaka huu na kuwa rapa wa kwanza kwenye orodha hio akiwa na wasanii kama Kenneth “Babyface” Edmonds, Jimmy Jam & Terry Lewis, Robert Lamm, Max Martin, James Pankow, na Peter Cetera.

Songwriters Hall Of Fame inatambua mchango wa waandishi wa muziki nchini Marekani.

Sherehe hizi za Songwriters Hall Of Fame zitakuwa za 48 na zinategemewa kufanyika June 15 Marriott Marquis Hotel mjini New York.

Tazama na Sikiliza Interview Za Kuburudisha Kwenye Channel Yetu,Bonyeza HAPA

Weka Comments Hapa

Open