Michezo

Jose Mourinho ; Sikuwa na ushawishi wowote katika usajili wa Romelu Lukaku

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Kocha Jose Mourinho amewafunga midomo Chelsea baada ya kusema hakuwa na ushawishi wowote katika usajili wa Romelu Lukaku kwenye klabu ya Manchester United.

Lukaku, alisajiliwa na Man United akitokea Everton kwa ada ya pound milioni 75 huku bado Chelsea walikuwa wakijipanga kumsajili staa huyu.

Mourinho ambaye amewahi kufanya kazi na Lukaku amesema Hakutumia ushawishi wake au historia yao kumsajili staa huyu, ila Man United walikuwa tayari kulipa pesa za Usajili kwa Everton , Mshahara wa mchezaji na pesa za Madalali waliohusika kwenye dili hilo katika muda sahihi.

Lukaku kwenda United kulimkasirisha kocha Antonio Conte ambaye muda huo alitaka bilionea mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich amsajili Lukaku ili kuchukua nafasi ya Diego Costa.

#SammisagoNEWS

 

Weka Comments Hapa

Open