Burudani

Rapa Juelz Santana ajisalimisha polisi baada ya kukutwa na bastola kwenye kiwanja cha ndege

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Rapa Juelz Santana ’36’ amejisalimisha polisi baada ya kukimbia alivyokutwa na bastola kwenye kiwanja cha ndege cha Newark Liberty Airport

Juelz Santana Aka LaRon James, alikimbia na kuacha mizigo yake kwenye kiwanja hicho cha ndege baada ya kuona bastola yake ikionekana kwenye mashine za usalama za X-ray na kuamua kurudi nje ya kiwanja cha ndege na kuchukua Taxi huku akiacha silaha hio aina ya 38 Caliber, leseni yake ya kuendesha gari na mabegi mawili.

Santana kafunguliwa mashtaka manne ambayo ni Kubeba silaha baada ya kuwa na rekodi ya kufungwa jela, kubeba silaha ndani ya ndege, kubeba silaha bila kibali na kukamatwa na dawa za kulevya.

Juel Santana hata pata dhamana mpaka kesi yake itakapo anza kusikilizwa.

Aslay Awajibu Wanaomlinganisha na Alikiba na Diamond! Amkana MX Carter kuwa Meneja wake!

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open