Burudani

Muhudumu afukuzwa kazi baada ya kuvujisha stori ya Justin Bieber kutibiwa sehemu zake za siri

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako
Muhudumu wa kike wa hospitali ya Northwell Health huko Long Island amefunguliwa mashtaka na managment ya Justin Bieber baada ya kuvujisha taarifa za afya za staa huyu.
Muhudumu huyu amevujisha siri kuhusu huduma aliyopewa Justin Bieber kwenye sehemu zake za siri inayosemekana kuwa ‘Korodani’ zake ziliumia akiwa anacheza mpira uwanjani.
TMZ imedhibitisha kuwa Justin alitembelea hospitali hio ya Northwell Health mwezi wa tano mwaka huu baada ya kuumia sehemu zake hizo za siri akicheza mpira wa miguu, wakili David H. Rosenberg anayemwakilisha Kelly Lombardo anasema mteja wake amefukuzwa kazi sababu ya kosa hilo.
Kelly Lombardo anasema hajawahi kuliona au kushika faili la Justin na ameonewa kufukuzwa kazi.
#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open