Burudani

Mahakama ya Juu Kenya yafuta ushindi wa Uhuru Kenyata

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Mahakama ya juu nchini Kenya imefuta ushindi wa Rais Uhuru Kenyata kwa uchaguzi uliofanyika tar 8 Agosti 2017, na kutaka uchaguzi huo urudiwe.

Hukumu hiyo imetolewa leo na jopo la majaji 6 ilirushwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari nchini Kenya, imesema uchaguzi huo utarudiwa baada ya siku 60.

Akisoma uamuzi huo Jaji Mkuu David Maraga amesema “Uchaguzi wa urais uliofanyika 8 Agosti, 2017, haukuandaliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, hivyo matokeo yake ni batili, Natangaza kwamba Bw Kenyatta hakuchaguliwa na kutangazwa kwa njia inayofaa, agizo linatolewa na kuagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa na kufanyisha uchaguzi mwingine kwa kufuata katiba na sheria katika kipindi cha siku 60″

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa tarehe 26 Agosti 2017, baada ya Muunganiko wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA) kuishtaki Tume ya Uchaguzi kufanya udanganyifu juu ya uchaguzi huo uliompa ushindi Uhuru Kenyata.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open