Burudani

Huto amini jinsi rapa Lil Wayne alivyowaboa mashabiki wake mjini Columbia.

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Mashabiki wa rapa Lil Wayne wasikitishwa na kitendo cha staa huyu kukataa kufanya show baada ya kuombwa yeye na watu wake kupita katika mashine ya kukaguliwa katika ukumbi wa Colonial Life Arena mjini Columbia, huko South Carolina.

Ripoti kamili inasema sababu kuu ya Lil Wayne kushindwa kuingia ukumbini ni kuwa, aligoma kupita kwenye vifaa vya kukaguliwa kwa ajili ya usalama.

Uongozi wa ukumbi huo wa ‘Colonial Life Arena’ umetoa kauli kauli kuhusu Lil Wayne kutofanya show nakusema “Usalama wa watu ni kitu muhimu sana kwao na baada ya Wayne kugoma kukaguliwa, hawakuwa na njia nyingine ya upendeleo kwa Wasanii kwa sababu waliogopa kuhatarisha maisha ya watu”

Mashabiki hawata rudishiwa pesa zao walizotumia kununua Ticket hizo sababu wasanii kama Cardi B, 2 Chainz na Tory Lanes walifanya show zao.
#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open