Burudani

Lil Wayne akiuka masharti ya daktari kwa kurudi studio siku chache baada ya kuanguka Kifafa

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Rapa Lil Wayne amekiuka masharti ya daktari kwa kurudi studio kurekodi muziki siku chache baada ya kuanguka Kifafa akiwa hotelini mjini Chicago.

Lil Wayne alionekana studio na mcheza kikapu wa NBA Damian Lillard wa ‘Portland Trail Blazers’ mjini Los Angeles, Kwenye picha hii palikuwa na ujumbe wa #Confirmed uliopelekea tafsiri kuwa amefanya wimbo na Lil Wayne.

Lil Wayne alianguka Kifafa wiki iliyopita na daktari alimruhusu kurudi nyumbani pakiwa na masharti ya kupumzika kwa wiki mbili au zaidi.

Lil Wayne alikuwa studio na producer  Scott Storch ambaye kupitia Instagram alithibitisha kuwa Afya ya rapa huyu ni salama kwa sasa na anaweza kufanya kazi.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open