Burudani

Kama Chris Brown, rapa Meek Mill ameanza kuwa mtoto mzuri

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Kama ilivyokuwa kwa Chris Brown toka mwaka jana alivyoanza kusafisha kesi zake zote na kuwa na rekodi safi, sasa rapa Meek Mill kupitia mawakili wake wameanza kazi hio.

Meek Mill amemaliza adhabu aliyopewa baada ya kukutwa na hatia ya kumshambulia mpiga picha mmoja kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa St. Louis.

Wakili wake Joe Tacopina amesema mteja wake alikubaliana na mwendesha mashtaka kuimaliza kesi hiyo kwa kufanya kazi za kijamii ambapo Meek amefanya kazi hizo na kumaliza adhabu yake kwa amani.

Meek amebakiza siku chache kumaliza adhabu nyingine ya kufanya kazi za kijamii na kutokama twa kwa kosa lolote ndani ya miezi SITA, Adhabu hii ilikuwa kwa kosa la kuendesha hovyo chombo cha moto ‘PIKIPIKI’, kuhatarisha maisha yake, ya watu na kusababisha kelele kwa jamii.
Alichosema BillNass kuhusu Colabo ya Diamond Platnumz X Rick Ross

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open