Habari

Picha, Madonna kaasili (Adopt) watoto wawili kutoka Malawi….

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Pop staa kutoka Marekani Madonna ameasili watoto mapacha kutoka Malawi. Shughuli hii kubwa iliyotakiwa kuchukua miezi 3 mpaka 7 imechukua wiki mbili tu kwa mujibu wa mahakama ya Malawi.

Madonna aliandikisha kuasili watoto hawa Esther na Stella mnamo January 25, ila hakupeleka karatasi hizo mahakamani ndio maana alikanusha taarifa hizo mwezi wa wa kwanza sababu bado hapakuwa na taarifa rasmi.

Kazi hio ya kuasili imechukua muda mfuppi zaidi wakati huu kutokana na Madonna kuifanya hii kazi tayari mara moja miaka kadha iliyopita na kwamba amekuwa akisaidia sana raia wa Malawi kwa misaada tofauti.

Serikali ya Malawi imetumamlezi mmoja aende na Madonna Marekani kamanjia ya kusimamia watoto hao kwenye huu wakati wa kubadilisha mazingira.

Mama wa watoto hao mapacha alifariki siku tano baada ya kujifungua na baba yao alishindwa kuwalea sababu tayari alikuwa na watoto 5.

Stella na Esther wenye miaka 4 hawana habari kuwa aliyewaasili ni mtu maarufu sana duniani.

#StoriByMellisa

Kwenye gari, Diamond alivyompokea Zari….

Tazama na Sikiliza Interview Za Kuburudisha Kwenye Channel Yetu,Bonyeza HAPA

Weka Comments Hapa

Open