Burudani

Ex wa Usher aliyeambukizwa malengelenge na staa huyu adai fidia ya dola milioni 20

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Siku chache baada ya Ex wa pili wa Usher kudai dola milioni 10 baada ya maisha yake kuhatarishwa na staa huyu kwa kufanya nae tendo la ngono bila kinga akiwa na ufahamu kuwa ni mgonjwa, sasa stori hii imepiga hatua nyingine.

Ex huyu amefanyiwa vipimo zaidi na imegundulika kuwa anaumwa gonjwa la ngomo alilosumbuliwa nalo Usher Raymond #Herpes au kwa kiswahili Malengelenge.

Mawakili wa Dada huyu wamefuta kesi yao ya awali na sasa wanadai dola milioni 20 baada ya kugundua dada huyu anaumwa Malengelenge na gonjwa hili alilipata kutoka kwa Usher Raymond.

Hivi karibuni Usher alilipa dola milioni moja ili kumaliza kesi yya mwaka 2012 ambapo Ex wake mwingine alipata ugonjwa huu kutoka kwake.
Bonge La Nyau Amlipa Baraka Da Prince Ili wafanye Colabo

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open