Burudani

Kwa mara ya kwanza katika historia ya muziki,Billboard imekubali kutumia VIEWS za Youtube kama kigezo cha mauzo bora ya Muziki.

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Kwa mujibuwa HITS Daily Double Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya muziki,Billboard imekubali kutumia VIEWS za Youtube kama kigezo cha mauzo bora ya Muziki.

Chati kubwa ya muziki na albums ya Billboard Hot 20o imekubali kuchukua Namba ya watazamaji wa kazi za wasanii kama sehemu na kigezo cha kuonyesha kuwa kazi za msanii zinauza na kitawekwa wakati album inaingia kwenye chati zao.

Mpaka sasa tunasubiri kuona wasanii wa nje watapokeaje hili swala ukizingatia wengi hufanya izuri sana kwenye Youtube kwa video zao na albums kusikilizwa sana.

Hapa YouTube itasaidia kuongeza namba kubwa ya mauzo ya muziki, kupunguza pesa nyingi wanazotumia wasanii kutangaza kazi zao,

Pia wakongwe wa muziki Marekani hawapendi jambo hili na tayari mmiliki wa lebo inayosimamia kazi za Kendrick Lamar  Top Dawg Entertainment CEO Anthony “Top Dawg” Tiffith alisema February 2016, hatupendi wanachofanya Recording Industry Association of America kuhesabu namba za watu waliosikiliza album mtandaoni ‘TIDAL, SPOTIFY’ kama sehemu ya mauzo, tupaki kwenye kununua album kama kigezo, uza album milioni moja , hapo nipehongera yangu.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open