Burudani

Nicki Minaj ametajwa kuwa shahidi katika kesi ya ubakaji inayo mkabili kaka yake Jelani Maraj.

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Nicki Minaj ametajwa kuwa shahidi katika kesi ya ubakaji inayo mkabili kaka yake Jelani Maraj.

Kwa mujibu wa Page Six, wakili wa Jelani ‘David Schwartz’ amesema kesi hii ni njama za kupata fidia ya dola milioni 25 kutoka kwa familia ya Nicki Minaj.

Mama wa mtoto anayelalamika kubakwa Jacqueline Robinson, alimwambia Nicki kuwa anaweza kufuta kesi kama watalipwa dola milioni 25.

Ndani ya siku chache tu baada ya Jacquelin kufunga ndoa na Jelani ndipo mtoto wake wa miaka 11 alianza kusema baba yake amembaka mara nne kila wiki.

Biti huyo alikuwa na miaka 8 alivyoanz kufanyiwa hivyo vitendo, DNA ya kaka yake Nicki Minaj ilikutwa kwenye nguo za kulala za mtoto huyo huku wakili wa Jelani akidai kuwa iliwekwa hapo na mama yake mzazi ili kupata pesa kutoka kwa Nicki Minaj.

Kaka yake Nicki amekataa mashtaka yote haya toka alivyokamatwa December 2015.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open