Burudani

Chrisette Michele aelezea alivyoteseka baada ya kufanya show kwenye sherehe ya kuapishwa Rais Donald Trump.

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Kwenye interview wiki hii staa wa R&B Chrisette Michele ameongelea alivyoteseka baada ya kukubali kufanya show kwenye sherehe za kuapishwa Rais Donald Trump.

Chrisette Michele ambaye ni muamerika mweusi alipondwa sana kwneye mitandao ya kijamii na hata kutengwa na familia yake baada ya kukubali kuimba kwenye sherehe ya Kuapishwa Rais Donald Trump.

Chrisette Michele anasema “Sikufikiria mara mbili nilivyopewa kazi hio, hapo hapo nilikubali kuimba, nilijua nitakutana naye na kuongea kuhusu niliyoyasikia kwneye kampeni zake na je kwanini anadhani ni sawa kuongea na sisi hivyo? ”

Hata hivyo Michele hakupata nafasi ya kukutana na Trump na kitendo cha yeye kufanya show hio kimepelekea muongozaji wa filamu Spike Lee kutoa wimbo wa Michele “Black Girl Magic” kutoka kwenye show yake ya “She’s Gotta Have It.”

Tazama na Sikiliza Interview Za Kuburudisha Kwenye Channel Yetu,Bonyeza HAPA

Weka Comments Hapa

Open